UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BEIJING, CHINA
MPANGO WA KUONDOKA KWA DHARURA
(EMERGENCY EVACUATION PLAN - EEP)
JUMLA
Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ambazo zimeshuhudia amani kwa miongo mingi. Hata hivyo, pamoja na amani hiyo iliyopo, Dunia imeshuhudia katika nyakati mbali mbali vurugu zikitokea katika nchi mbalimbali na kusababisha mamia ya watu kupoteza maisha na mali kuharibiwa. Vuguvugu la kisiasa, mabadiliko ya utamaduni au mfumo fulani wa maisha vinaweza kusababisha kutokea vurugu katika nchi yo yote, ambazo zinaweza kupelekea kutoweka kwa amani katika nchi hiyo na hivyo kulazimisha nchi zenye wanadiplomasia au raia nchini humo, kuondoa watu wao pamoja na raia wa nchi rafiki kwa dharura. Hayo yameshuhudiwa mwanzoni mwa mwaka wa 2011 katika nchi za Kaskazini mwa Afrika za Tunisia, Misri na Libya ambapo nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania zililazimika kuondosha raia wao kwa dharura kwa usalama wao.
Tafadhali,download na soma kwa ufasaha nakala kamili ya mpango huu inayopatikana HAPA