tz embassy

 Photo Gallery  |  Links  |   Contact Us  |   Email Alertiiii
Beijing:
Dar es Salaam:

Tanzania Passports – Information and Procedure

 

A. UTARATIBU WA KUPATA PASSIPOTI MPYA

Baada ya maulizo mengi kuhusu utoaji wa Pasipoti Mpya, ufuatao ni utaratibu wa kushughulikia zoezi hilo katika nchi za uwakilishi wetu*:

A. Utaratibu wa Kupata Pasipoti Mpya

 1. Mwombaji anaweza kuja Ubalozini na pasipoti aliyonayo ili kununua fomu (malipo ya fomu ni USD 10) pamoja na kopi mbili za pasipoti aliyonayo kurasa za 1 hadi 5 na ukurasa wa mwisho wenye DN. Namba. Aidha, alete bahasha yenye anuani yake iliyobandikwa stampu za rejista ili apelekewe fomu.

 1. Malipo yakipokelewa, mwombaji atapewa fomu au atapelekewa fomu husika ambayo ataijaza BILA kuweka sahihi yake katika sehemu ya sahihi, ukurasa wa kwanza. Mwombaji ataileta fomu yake, `photocopy' ya fomu iliyojazwa na picha tano (5) za pasipoti saizi ya 4 x 4.5 cm zenye `background' ya rangi ya `sky blue' au rangi ya maji ya bahari. Picha hizo lazima ziwe za karibuni sana zinazoonyesha masikio yote mawili.


*FOMU IJAZWE KWA HERUFI KUBWA!

 1. a) Wakati wa kujaza fomu `Section 2' tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa wazazi ni LAZIMA. Hata wazazi waliofariki.

b) Kama kuna sababu ya kubadilisha jina lazima hati husika za sababu ya kubadili jina ziletwe - k.m. cheti cha ndoa.

c) Kama pasipoti imepotea LAZIMA ripoti ya polisi na `affidavit' (hati ya kiapo) mbele ya mwanasheria zitumwe pamoja na fomu na maelezoo ya kina ya mazingira ya kupotea kwa pasipoti hiyo, yatakayoweza kuusaidia Ubalozi kuyaamini.

Wale watakaopenda kuja Ubalozini kununua fomu na kurudisha fomu wazingatie utaratibu ulioelezwa (1 - 3).

d) Acha au usijaze kipengele cha sita (6) katika fomu kwa kuzingatia Maelezo Muhimu kwenye kipengele cha pili (2) - waliotajwa hawapatikani nje ya Tanzania.

e)Kila fomu ina namba moja haitumiki kwa watu wawili. Mwombaji asithubutu kutoa nakala (photocopy) ili itumike kwa mwombaji mwingine.

 1. Inatahadharishwa kuwa fomu za uombaji pasipoti zilizokosewa au kufutwafutwa hazitakubalika na itabidi mwombaji anunue fomu nyingine. Ni vema kabla ya kujaza fomu mwombaji atoe nakala (photocopy) ya fomu aijaze kwanza kila kipengele ili baadaye anakili katika fomu aliyopelekewa kuepuka makosa, kufutwafutwa na kununua fomu nyingine.

B. Alama za Vidole na Tahadhari

 1. Katika utoaji wa pasipoti mpya lazima mwombaji achukuliwe alama za vidole (`finger prints') na kuweka sahihi kwa mkono wake mwenyewe mbele ya afisa mhusika. Hivyo, tarehe ya kuchukuliwa alama za vidole; mwombaji atajulishwa kwa simu au e-mail.

 1. Mwombaji LAZIMA aje UBALOZINI ili kutia sahihi fomu na kuchukuliwa alama za vidole. Mwombaji atatakiwa alipe USD 40- malipo ya pasipoti mpya.

 1. Maombi yatashughulikiwa ipasavyo na kupelekwa haraka Makao Makuu ya Uhamiaji Dar es Salaam katika mfuko maalum wa Kidiplomasia.

 1. Pasipoti mpya zitatolewa Makao Makuu ya Uhamiaji, Dar es Salaam na zitaletwa Ubalozini kwa mfuko maalum.

 

 1. Ubalozi utatuma pasipoti mpya kwa mwombaji kwa kutumia bahasha iliyoandikwa anuani na mwombaji na kuwekwa stampu za rejista. Pasipoti ya zamani itabidi iwe ′cancelled' ili nayo irudishwe kwa Mwombaji katika bahasha moja na pasipoti mpya. Hivyo, mawasiliano na Ubalozi ni muhimu kwani pasipoti mpya haitatolewa kabla ya ile ya zamani kuwa `cancelled'. Watakaotaka kufuata pasipoti zao wenyewe ni ruksa.

 1. Utaratibu mzima wa kushughulikia unatazamiwa kuchukua wiki sita (6) au zaidi. Jumla ya gharama ni USD 50- yaani USD 10- za fomu na USD 40- pasipoti.

 

*ANGALIZO:


(i) Pasipoti mpya zitatolewa kubadilisha zile ambazo ni halali na zenye kumbukumbu za utoaji kwa raia wa Tanzania. Siyo kwa wale wenye uraia wa nchi nyingine walio na pasipoti mbili. Kisheria nchi yetu hairuhusu `uraia wan chi mbili; kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. Akigundulika mwombaji mwenye uraia wa Tanzania na nchi nyingine atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

(ii) Watoto watapewa pasipoti zao kwa kuzingatia utaratibu ulioelezwa.

Watoto wa umri usiozidi mwaka mmoja hawatachukuliwa alama za vidole - wengine zaidi ya mwaka mmoja lazima wachukuliwe alama za vidole.

(iii) Watanzania wanaokwenda nyumbani siku za karibuni wanashauriwa na wanaruhusiwa kuomba pasipoti mpya wakati wakiwa nyumbani katika ofisi za Uhamiaji Tanzania. Kufanya hivyo kutawaharakishia kupata pasipoti hizo.

(iv) Ubalozi wetu unashughulika pia na nchi za Vietnam, Thailand, Laos, Cambodia, Mongolia na Korea Kaskazini.

 

C. Kujumuisha Watoto Katika Pasipoti ya Mzazi


Kwa utaratibu wa pasipoti mpya, watoto wadogo au walio chini ya umri wa miaka 18 hawataingizwa katika pasipoti za wazazi. Kila mtoto itabidi aombewe pasipoti yake mwenyewe.

 

Waliopoteza Pasipoti


Kwa waliopoteza Pasipoti, LAZIMA kuwasilisha pamoja na maombi yako vifuatavyo:

 • Ripoti ya polisi kuthibitisha kupotea/kuibiwa kwa Pasi ya Mwombaji
 • Mwombaji atoe maelezo binafsi kwa maandishi akieleza yafuatayo:
 • Taarifa za Pasipoti iliyopotea,
 • Mazingira ya upoteaji wa Pasipoti,
 • Mahali Pasipoti ilikopotelea
 • Tarehe na mwaka Pasipoti ilipotolewa, Namba ya Pasipoti na DN.
 • Taratibu za kawaida za kuomba Pasipoti zitafuata baada ya Mwombaji kukamilisha maelekezo ya hapo juu.
 • Ni juu ya mwombaji kutafuta taarifa hizo, na kuufanya Ubalozi uamini maelezo yake. Kwa mtu asiye na uthibitisho wowote ni vigumu kwetu kumpa huduma hiyo.

 • Ukishindwa kabisa ni vyema ukawasiliana na wazazi huko nyumbani ili wapeleke uthibitisho huo Uhamiaji Makao Makuu kwa msaada zaidi.
Rate this item
(2 votes)

Contact Us

Address: 8 Liang Ma He Nan Lu, Sanlitun, 100600 Beijing, P. R. CHINA.
TEL: (+86) 010 65321719
FAX: (+86) 010 65324351
E-mail: beijing(at)nje.go.tz

Visitors Counter:  joomla statistics